DKT. GWAJIMA: “MHE. RAIS AMETUHESHIMISHA KUWALETA MACHINGA KATIKA WIZARA YETU, TUTASHIRIKIANA KATIKA MAENDELEO”

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewaheshimisha sana kama Wizara, mara baada ya kulitambua kundi la Machinaga kama kundi maalum, na kuliweka chini ya Wizara hiyo ili kero zao ziweze kutaliwa kwa haraka na kwa wakati.